Announcements

 • Maelekezo CODIV-19

  Announced by Almodad Amos on Apr 17 2020

  TANGAZO KUHUSU TARATIBU ZA IBADA WAKATI WA COVID-19

  Tafadhali rejea, tamko lifuata kutoka kwa Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania:

  Kufuatia tangazo hili, Ofisi za Konferensi NETC zinapenda kuwajulisha kuwa kesho siku ya Sabato ya Tarehe 18 Aprili 2020, tutaungana na Watanzania wengine (Huku tukiendeleza siku 100 za maombi) katika kumuomba Mungu kutuondolea na kutuepusha na Janga hili la Covid-19.
  Pia tarehe 25 Aprili 2020, itakuwa siku maalum ya NTUC kufanya maombi maalum kwa ajili ya hili janga la Covid-19. Hiyo ya kwanza tunaungana na Watanzania wote ktk maombi, na hii ya pili ni Program ya Kikanisa. Tafadhali zote mbili zipewe uzito.
  Pia Ofisi za NETC zinaendelea kutoa na kukumbushia maelekezo kuhusiana na kujikinga na kujiepusha na hatari ya Ugonjwa huu:
  Ibada zetu makanisani ziwe fupi na zisivuke saa sita kamili.

  Matangazo makanisani yawe mafupi sana kadri inavyowezekana.

  Ushauri kutoka Idara ya Mawasiliano
  Kama inawezekana makanisa yatumie njia ya machapisho, mitandao ya kijamii pamoja na SMS ili kufikisha matangazo kwa Washiriki na ule muda wa matangazo tutakuwa tumefanikiwa kuufupisha huku matangazo yakiwa yamefika kwa wakati.

  Mjadala wa Mwongozo wa Kujifunza Biblia pale inapolazimu ili kuepuka kukaa muda mrefu Kanisani, hebu na usimamiwe na mtu mmoja akiwa kama mwenyekiti wa mjadala. Ikiwa watu watakwenda ktk mgawanyiko, pawe na watu wa kuelekeza na watakavyoketi kwa kupeana nafasi watu wanaporejea kutoka katika vikosi vyao.

  Maelekezo ya usafi kama yalivyotolewa na mkurugenzi wa Afya, Dkt. Amos Kihedu, hebu yaendelee kufuatwa na kupewa uzito mkubwa.

  Kila mmoja wetu anaalikwa kuendelea kumuomba Mungu kutuandaa kwa ujio wake maana hii ni moja kati ya dalili kwamba anakuja na pia tumuombe awasaidie watu kuepukana na hatari hizi zinazoletwa na yule mwovu.

  Ujumbe huu unakuja kwetu kutoka Ofisi ya Mwenyekiti na katibu Mkuu NETC.