Utume Wetu

TAMKO LA UTUME WA KANISA
Utume wa Kanisa la Waadventista wa Sabato  ni kuwaalika watu wote wawe wanafunzi  wa Yesu, kutangaza Injili ya milele katika muktadha wa Ujumbe wa Malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12, na kuuandaa ulimwengu kwa marejeo ya Kristo yaliyo karibu.

UTEKELEZAJI WA UTUME WETU
Kwa kuongozwa na Biblia na Roho Mtakatifu, Waadventista wa Sabato hutekeleza utume huu kupitia maisha yanayoakisi alivyoishi Kristo, katika kuwasiliana, kufanya wanafunzi, kufundisha, kuponya, na kuhudumia.

NJOZI YA UTUME WETU
Kwa kupatana na mafunuo ya Biblia, Waadventista wa Sabato tunauona utume wetu ukifikia kilele katika mpango wa Mungu wa urejeshwaji wa viumbe vyake katika ukamilifu wa mapenzi yake na haki yake.

TAMKO LA UTAMBULISHO NA UTEKELEZAJI WA UTUME WETU

UTAMBULISHO WETU
Kanisa la Waadventista wa Sabato linajitambua kuwa ni Kanisa la masalio la unabii wa Biblia wa siku za mwisho. Washiriki wa Kanisa hili, mmoja mmoja au kwa pamoja, huelewa  jukumu lao maalumu kama mabalozi wa ufalme wa Mungu,  na wajumbe wa marejeo ya Yesu Kristo yaliyo karibu. Waadventista Wasabato wamejiandikisha kama jeshi la wafanyakazi pamoja na Mungu katika utume wa kuurejesha ulimwengu kutoka katika nguvu na uwepo wa uovu, kama sehemu ya Pambano Kuu baina ya Kristo na Shetani. Kwa hiyo, kila hali ya maisha ya mshiriki wa Kanisa huathiriwa na kusadiki na kuamini kuwa tunaishi katika siku za mwisho za unabii wa Biblia na kwamba kurudi kwa Yesdu Kristo kuko karibu sana.Waadventista Wasabato wameitwa na Mungu kuishi katika ulimwengu huu.Kila tendo la maisha ya Mkristo hufanyika “katika jina la Yesu” na kutangaza ufalme wake.

UTEKELEZAJI WA UTUME WETU
Waadventista wa Sabato hukiri kwa dhati kuwa Maandiko Matakatifu, Biblia, ni ufunuo wa mapenzi ya Mungu usio na makosa, hukubali mamlaka yake (Biblia)  katika maisha ya Kanisa na ya kila muumini, na kwamba ndicho kipimo cha imani na mafundisho.  Waadventista wa Sabato huamini kwamba Roho Mtakatifu ndiye uwezo unaobadili maisha yetu mwenye kuwapatia watu vipaji vya kutangaza ufalme wa Mungu katika ulimwengu huu.

Wakiwa wameitwa na Mungu, na kuongozwa na Biblia, kwa kuwezeshwa na Roho Mtakatifu, Waadventista wa Sabato, kokote tunakoishi ulimwenguni, kwa moyo wa kupenda kufanya kazi hujitoa kufanya yafuatayo:

Kuishi kama alivyoishi Kristo
Kadri tunavyoishi tutaonesha kuwa Kristo ndiye Bwana wetu kimaadili, kiutamaduni na kimwenendo katika jamii, kwa kuongozwa na mafundisho yake muda wote na tukiiga mfano wake.

Kuwasiliana kama alivyowasiliana Kristo
Tukielewa kuwa sote tumeitwa  tushuhudie kwa nguvu, tunashiriki  kwa njia ya mazungumzo binafsi, mahubiri, uchapishaji na stadi mbalimbali,  ujumbe wa Biblia juu ya Mungu, tumaini tulilonalo na wokovu uliotolewa naye kupitia maisha, utume, kifo, ufufuo na huduma ya ukuhani wa Yesu Kristo. 

Kufanya wanafunzi kama alivyofanya Kristo
Kwa kuthibitisha ukuaji wa kiroho ulio endelevu kwa maendeleo ya waumini, tunatoa malezi kwa waumini wapya, tukiwafunza kuishi maisha ya haki na kuwaelekeza kushuhudia kwa mguso wenye nguvu na kuwatia shime kuonyesha mwitikio wa utii kwa mapenzi ya Mungu.

Kufundisha kama alivyofundisha Kristo
Tukikiri kwamba maendeleo ya mwili na tabia ni vya muhimu katika mpango wa Mungu wa Ukombozi, tunahimiza ukuaji katika kumwelewa Mungu na jinsi ya kuhusiana na Yeye, na Neno lake, pamoja na vitu vyote alivyoviumba. 

Kwa kuzithibitisha kanuni za Biblia za kuwa na utu wote mkamilifu
Tunafanya utunzaji wa afya zetu na uponyaji wa wagonjwa kuwa kipaumbele chetu.  Kwa kuwahudumia maskini na wanaoteseka, tunashirikiana na Muumba katika kazi yake ya urejeshwaji kwa njia ya matendo ya huruma.

Kutumika kama alivyotumika Kristo
Kwa kufuata kielelezo cha Yesu tutajitoa kuwa na utumishi wenye unyenyekevu, tukiwahudumia watu na jamii za watu walioathiriwa zaidi na umasikini, misiba, wasio na matumaini na wagonjwa