Mawasiliano


KARIBU KATIKA IDARA YA MAWASILIANO

Idara ya mawasiliano, ni chombo muhimu sana katika Kanisa la Bwana, hasa katika wakati tunaoishi ndani yake sasa. Jaribu kutafakari maneno haya: Kwamba karibu karne mbili zilizopita, jambo kubwa katika fikra za wanadamu ilikua ni kuisaka mali na pesa. Katika zama tulizonazo sasa mambo yamebadilika kabisa, jambo lililo muhimu sana imekuwa ni kupata habari kupata habari.


FALSAFA YA MAWASILIANO

Mawasiliano ni njia inayotumiwa na viumbe hai ili Kubadilishana, Kufahamishana, Kujulishana au kutaarifiana mawazo, habari au hisia kutoka kwa mtu/kundi moja kwenda kwa mtu mwingine au kundi jingine. Kwa mujibu wa Biblia, katika siku hizi za mwisho kanisa litapaswa kuhusika sana na HABARI.... “Tena habari njema ya ufalme itahubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; hapo ndipo ule mwisho utakapokuja. Mathayo 24:14”

Mungu wetu mwenye uwezo wa kuona mambo yajayo kabla hayajafika na kutangaza mwisho tangu mwanzo (Isaya 46:10), aliyaona maendeleo haya ya teknoljia ya mawasiliano tangu hapo mwanzo na hivyo akasema watu wa siku za mwisho, pia, wangalihabarishwa juu ya ufalme wa Mungu, ufalme uliojaa neema na pendo la Mungu kwa wanadamu. Katika kuhabarishana huku, nabii Danieli alieleza kwa undani zaidi kwamba maarifa yangeongezeka (Dan 12:4) na sasa ni jambo ambalo liko wazi kabisa kwamba maarifa yameongezeka katika nyanja nyingi na hasa katika nyanja ya teknolojia ya mawasiliano. Hivyo basi, swala la matumizi ya njia za kisasa katika kuwahabarisha wakazi wa ulimwengu huu juu ya ufalme wa Mungu, ni jambo lisiloepukika hata kidogo.

Ellen G. White aliandika: “Njia zitabuniwa ili kufikia mioyo. Baadhi ya mbinu zinazotumika katika kazi zitakuwa tofauti na mbinu zilizotumiwa katika siku za nyuma” (Evangelism uk 105). Idara ya mawasiliano huhamasisha utumiaji wa programu thabiti ya uhusiano na mbinu zote za kisasa za mawasiliano, tekinolojia endelevu na vyombo vya habari katika kueneza injili... Mwongozo wa kanisa (Toleo la 2010) uk 104.

Idara ya mawasiliano huhimiza matumizi ya programu timamu ya mahusiano na umma na aina zote za ufundi wa mawasiliano ya kisasa, tekinolojia endelevu na vyombo vya habari katika utangazaji rasmi wa injili ya milele. Kwa maelezo zaidi tembelea Ukurasa wa semina kisha  bofya "Download" Semina ya Idara ya "Mawasiliano" ili kupata maelezo zaidi kuihusu Idara ya mawasiliano NETC, na jinsi inavyofanya kazi.

MISISITIZO MIKUU YA IDARA YA MAWASILIANO

  • Kuanzisha Studio za Hope Media NETC: Sasa hivi Konferensi inaendelea na zoezi la ujenzi wa Studio ambayo itafanyakazi kamatawi la TAMC.
  • Kuhimiza watu viongozi na wadau wa Mawasiliano kuhudhuria mkutano wa GAiN
  • Kutengeneza miongozo kwa viongozi wa Idara ya mawasiliano kanisani
  • Kukusanya semina mbalimbali na kuziweka kwenye mtandao ili zitumike kama zana za utume kwanza
  • Kutumia mitandao ya kijamii katika kuwasiliana na waumini wa Kanisani na kufanya uinjilisti
  • Kuandika machapisho mbalimbali yanayohusu shughuli za utume na kuyatuma kwa wahusikA
  • Kuzitengenea Idara nyingine nyenzo za kupeleka mafunzo, semina na miongozo kwa makanisa mahalia.
  • Kuhakikisha kuwa tunatoa kalenda ya matukio.

ZINGATIA YAFUATAYO
  • Kwa maoni zaidi au maswali, tafadhali tuandikie kwa mrindokoa@netcadventist.org au piga simu namba 0719 184 313