Announcements

 • Maelekezo ya Mafundisho Makuu ya Makambi 2022

  Announced by Almodad Amos on Jul 11 2022

  Ujumbe Huu Unatoka Katika Ofisi ya Mwenyekiti NETC

  Wapendwa Wahudumu Wote wa Makambi NETC 2022 nawasalimu katika jina la YESU KRISTO na hongereni sana kwa makambi yaliyomalizika na yanayoendelea. 

  Kwa kuwa pamekuwa na changamoto na upandikizwaji potofu hasa kwa FUNDISHO LA ROHO MTAKATIFU, ikiwa ni Pamoja na kudhani kuwa Roho Mtakatifu si MUNGU, siyo NAFSI, na hakuna UTATU MTAKATIFU, na kwa kuwa kama Konferensi tumeelekeza kuwa Kipindi cha Mafundisho Makuu, Fundisho hili lifundishwe kwa Kina, Undani, Uwazi,  na Kueleweka, na kwa kuwa kuna Somo maalumu lililoandaliwa na Idara ya huduma za Kichungaji kama Mwongozo na kupitiwa na Wanatheologia Wabobezi, na kwa kuwa imeonekana baadhi ya Wahudumu hawafundishi kama maelekezo ya Konferensi, Naomba kuelekeza yafuatayo:
  1. Kila Mhudumu anayehusika na kipindi hiki ahakikishe anafundisha Fundisho hili la ROHO MTAKATIFU kama Maelekezo ya Konferensi.
  2. Mhudumu husika anaelekezwa apitie kitini hiki chenye kurasa 13 cha somo hili kwa kina na kuelewa kabla ya kufundisha,
  3. Mhudumu ASIHUBIRI bali AFUNDISHE na atumie maswali yaliyowekwa kila siku kama Njia ya kuamsha fikra za washiriki huku akiacha muda wa Washiriki Kuuliza Maswali na kuongeza.
  4. Mhudumu anaelekezwa kufuata Utaratibu ulioelekezwa kwenye ukurasa wa Utangulizi ikiwa ni Pamoja na mgawanyo wa zile Dakika 60 za kipindi chake (Utangulizi, Maswali kwa Wasikilizaji, Somo lenyewe, Maswali kutoka kwa wasikilizaji na Hitimisho),
  5. Kila Wahudumu wa kituo cha Kambi na Mchungaji mwenyeji washirikiane kwenye ufafanuzi hasa wakati wa Maswali na Mjadala,
  6. Kila Mchungaji alitumie somo hili kuendelea kufundisha Fundisho hili la Roho Mtakatifu kwa washiriki wake hata baada ya Makambi,
  7. Na mwisho namuelekeza Mratibu wa Makambi kufatilia kwa ukaribu utekelezaji wa jambo hili kwa maslahi mapana ya Kulilinda kanisa na Mafundisho yake, 
  Asanteni sana kwa ushirikiano wenu, nawatakia Makambi mema.
  Mch. Musa Nzumbi- Mwenyekiti NETC