North East Tazania Conference inahudumia Jiografia ya Mikoa miwili yani Kilimanjaro na Tanga na sehemu ya Wilaya ya Simanjiro (Tarafa za Ruvu Remit, Msitu wa Tembo na Moipo).

Sisi ni sehemu ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ambayo ni jamii ya watu waliokusudia kwa nia moja, kukuza uhusiano wa karibu kabisa na Mungu wao na kuwa na mwenendo kama aliokuwa nao Yesu. Kiini cha utume wetu ni kuushuhudia ulimwengu juu ya tumaini pekee lenye baraka linalotokana na uzoefu binafsi wa mahusiano bora na Mungu Mwokozi wetu mwenye Upendo, na kujiandaa kwa tukio kubwa kabisa la marejeo yake ambayo yamekaribia sana.