Ndugu Mjumbe wa Mkutano Mkuu,
Karibu kwenye Mkutano Mkuu wa Nane (8) wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Konferensi ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania (NETC), unaofanyika hapa Makao Makuu ya NETC, Same- Kilimanjaro, siku ya Jumatatu, 22 Septemba 2025.
Neno Kuu la Mikutano hii ni “YESU ANAKUJA NITAKWENDA”, “PAMOJA NA YESU NITAKWENDA ZAIDI YA KAWAIDA” ndiyo Kaulimbiu yetu Kuu katika Konferensi yetu 2021-2025 inayotuhimiza kwenda Zaidi ya kawaida katika nyanja zote za kazi ya Mungu na umuhimu wa ushirikishwaji wa kila Mshiriki na kuandaa wengine waokolewe.
Huu unakuwa Mkutano Mkuu wa Pili kufanyika baada ya Konferensi yetu kugawanywa na kubaki na Mkoa wa Kilimanjaro na Tanga pamoja na sehemu wa wilaya ya Simanjiro.
Kwa kawaida, Mkutano Mkuu hutoa fursa kwa Familia ya Waumini ya Kanisa katika Konferensi nzima kukutana pamoja kwa ajili ya Ibada na kujumuika Pamoja katika Kutathmini Kazi ya kipindi cha Mhula uliopita, kupanga kazi kwa Mhula unaofuata, Kuchagua Viongozi na kupitisha mambo muhimu yanayolihusu kanisa na taasisi zake. Kwa sababu hiyo, Mkutano huu wa Nane utatoa tathmini ya Kazi kwa miaka Mitatu (3) tangu June 2022 hadi June 2025, na utaweka Mipango ya kazi kwa miaka ijayo Mitano (5) ya 2025-2030.
Kwa niaba ya Familia yote ya NETC, nakukaribisha sana wewe mjumbe kushiriki kikamilifu katika mkutano huu Ungana nami kuombea Uongozi wa MUNGU kwa ratiba hii muhimu ya Kihistoria kwa Konferensi yetu. Nikukaribishe tena karibu, na nakutakia ushiriki wenye mafanikio, afya njema na baraka tele za Mungu.
Mwenyekiti wa NETC
Musa E. Nzumbi