Mfumo wa Utambulisho wa Kanisa

Tunazungumza lugha tofauti. Sisi huvaa kwa namna tofauti tofauti. Tuna kazi tofauti. Mitindo tofauti. Tunaishi katika nchi, tamaduni, na vitongoji tofauti. Tunamwabudu Mungu kwa njia tofauti tofauti. Sisi sote tunasheherekea wokovu wetu, wote tunamkiri Yesu kama Bwana na Mwokozi wa maisha yetutunashangilia furaha, kwa njia tofauti, naam njia ma-milioni. Zaidi kuliko yote, sisi sote ni Waadventista Wasabato

Haya yanadhihirika katika jina letu lenye msisitizo wa Utunzaji wa Sabato ya siku ya Saba, na Taraja ya matumaini ya kurejea kwa Yesu. Historia yetu na harakati zetu zimezingatia ufahamu wa wakati tulionao sasa, na umuhimu wa unabii wa ujumbe wetu katika masaa haya ya mwisho ya historia ya dunia. Sisi ni watu tofauti, kama ukiangalia nyuma katika historia na huko mbele tunapoelekea; tumeitwa kushiriki na kila mtu kwamba dunia iko karibu na ukingo wa mwisho wa uzuri.

Haijalishi tuko wapi, mashirika yetu yanaonekana namna gani, jinsi tunavyoiishi imani yetu, na jinsi tunavyoendelea kuitunza Sabato, sisi sote tunatamani siku hiyo ya mwisho ambapo hatimaye tutakuwa pamoja na Mungu wetu.

Tuna tumaini hili, na tangu mwanzo wetu tumezungumza, kuchapisha, kuzalisha, na kutengeneza vyenzo mbalimbali za kushirikiana na wenzetu juu ya tumaini hili. Lakini sasa, hatukuwa na mkakati wa umoja wa jinsi ya kuonyesha maelfu ya nyezo ambazo tumekuwanazo katika kulingaza tumaini hili.

Makanisa yetu, maidara, na mashirika yamekaa muda mrefu sana yakijaribu kusimama, lakini bado inaweza kuwa vigumu kwa watu wanaotutazama kutuambia kuwa wote sisi tumesimama kwa umoja na pamoja. Katika kujitegemea wenyewe, wakati mwingine tulisahau kufikiri juu ya mazingira yetu na nini kinachoweza kuwasaidia wasikilizaji wetu kujua sisi ni sehemu ya mwili mmoja. Kwa kadri ulimwengu unasumbuliwa na kusongwa na habari, na wakati walengwa wa habari wanapotafuta njia zao wenyewe za kupata habari inayoeleweka, na kadri wazalishaji wa maudhui wavyo endelea kujaa katika soko la habari, ni muhimu kwetu leo kutafuta njia ya kuwasaidia watu kujua sisi ni Wadventista wa Sabato (na hatujagawanyika).

Sasa basi tunawezaje kujitambulisha wenyewe? Tunawezaje kutumia rangi, chati, picha, na mipangilio ya Sanaa ya uandishi ili kuwawezesha watu kujua wanaangalia vitu vya Waadventista? Tunawezaje kuanzisha mfumo unaounga mkono idadi ya kuongezeka ya miundo, nyenzo, na vifaa vya utangazaji wa neno la Mungu? Jambo la muhimu zaidi, je, tunawezaje kuunda mfumo rahisi wa kutosha kushughulikia utofauti wetu, huku tukijitolea wenyewe kama mwili umoja?

Baada ya miezi kadhaa ya maombi, maswali haya magumu, kwa kupima mbinu tofauti, na kushirikiana na wanamawasiliano wa Kanisa ulimwenguni kote, tumeanzisha mfumo tunaoamini unaweza kufikia malengo yetu ya kuunga mkono umoja wetu katika utofauti wetu. Ni imani yetu thabiti kuwa ushiriki wa kimataifa katika mfumo huu wa maisha, wa utambulisho wa nguvu utasaidia katika kuzitangaza habari njema za ujumbe wa Marejeo kwa njia zenye ufanisi mzuri na zitakazopokelewa na wapokeaji habari tunazopeleka sokoni.

NETC imeandaa mwongozo maalum ili kusaidia makanisa na taasisi kulitambulisha Kanisa na kile linachoamini kwa namna ambayo itasaidia kuliweka Kanisa katika utambulisho unaoeleweka. bofya HAPA