Wachungaji Wawekewa Mikono

Posted on Oct 01 2018


Na Almodad Amos

Habati NETC | Moshi

Sabato ya tarehe 29 Oktoba 2018 itakuwa sabato ya kukumbukwa sana katika historia ya Mch. Jackson Mding'i na Mch. Daniel Gitianga ambao wamewekewa mikono ya kutengwa kwa kazi maalum ya kichungaji (Kuwekwa wakfu) katika ibada ya sabato hiyo ambayo mnenaji na mgeni rasmi alikuwa Mchungaji na Daktari Godwin Lekundayo - Mwenyekiti wa Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania.
Akizungumza na umati wa waumini wa Kanisa la Waadventista Wasabato waliojidhurisha katika ibada hiyo takatifu, ameliasa Kanisa na hasa Wachungaji kuachana na tabia ya ubaguzi wa aina yoyote katika utoaji wa huduma za kichungaji bila kujali itikadi, kabila, lugha au tabaka la mtu.