01. Maandiko Matakatifu

MAANDIKO MATAKATIFU

 “Maandiko Matakatifu, Agano la Kale na Agano Jipya, ni Maandiko ya Mungu yaliyoandikwa, yaliyotolewa kwa kuvuviwa wanadamu watakatifu wa Mungu ambao walinena na kuandika kwa kuongozwa na Roho Mtakatifu. Katika Neno hilo, Mungu amewapatia wanadamu ujuzi muhimu kwa wokovu. Maandiko Matakatifu ni ufunuo usiokosea wa mapenzi yake Mungu. Ndicho kiwango cha tabia, kipimo cha uzoefu, mfunuaji mwenye mamlaka wa mafundisho na kumbukumbu ya kuaminika ya matendo ya Mungu katika historia.” (2Pet.1:20, 21; 2Tim.3:16, 17; Zab.119:105; Mith. 30:5, 6; Isa.8:20; Yoh. 17:17; 1Thes. 2:13; Ebr.4:12)

Hakuna  kitabu  ambacho  kimepata kupendwa, kuchukiwa, kuhofiwa, kushutumiwa kama Biblia. Watu wamekufa kwa ajili ya Biblia. Wengine wameua kwa ajili yake. Imehamasisha matendo makubwa na ya maana ya mwanadamu, na imelaumiwa kwa matendo maovu ya wanadamu.   Vita vimepiganwa kwa ajili ya Biblia, mapinduzi yamepangwa kwa kusoma kurasa zake, falme zimeangushwa kupitia fikra zake. Watu wa kila namna, wanathiolojia kwa mabepari, mafashisti kwa wafuasi wa Karl Max, madikteta kwa wakombozi, wapenda njia za amani kwa wapiganaji wa kivita, wote hujifunza maandiko kuhalalisha matendo yao.

Tofauti ya Biblia, haitokani na kule kutokulingalishwa kwake na mivuto ya kisiasa, kiutamaduni, na kijamii bali kutokana na jinsi ilivyo na inachofundisha. Ni ufunuo wa Mungu– Mtu pekee, Mwana wa Mungu, Yesu Kristo, Mwokozi wa Ulimwengu.

Ufunuo wa Mungu

Wakati katika historia wako waliohoji kuwepo kwa Mungu, wako wengine walioshuhudia yupo na amejifunua mwenyewe. Ni jinsi gani amejifunua na jinsi gani Biblia inazungumzia katika kujifunua wake?

Ufunuo wa kiujumla

Wazo juu ya tabia ya Mungu ambayo historia, tabia ya mwanadamu, dhamiri na uumbaji huitwa ufunuo wa kiujumla kwa kuwa unapatikana kwa wote na huvutia kwenye fikra. Kwa mamilioni ya wanadamu, mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu na anga latangaza kazi ya mikono yake (Zab.19:1). Mambo yake yasiyoonekana, sasa yako dhahiri na wanadamu hawana udhuru (Rum. 1:20). Wengine humwona Mungu katika mahusiano kwa upendo wa kirafiki, kifamilia, mume na mke, wazazi kwa watoto. (Isa.66:13; Zab. 103:13). Hata hivyo jua laweza kuunguza nchi ikawa jangwa, mvua yaweza kuleta mafuriko, ardhi yaweza kupata ufa, kuanguka na kuvunjia. Mahusiano ya wanadamu hujaa wivu, kijicho, hasira, chuki na hata kuleta maafa. Ulimwengu unaotuzunguka hutupatia ishara zinazosigana na kuleta maswali mengi kuliko majibu. Huonyesha pambano baina ya wema na uovu lakini havisemi kwa vipi na kwa nini pambano lilianza, nani anapigana kwa nini na ni nani ambaye hatimaye atashinda.

Ufunuo Maalum

Dhambi inaficha kujifunua kwa Mungu kupitia kazi yake ya uumbaji kwa kuzuilia uwezo wetu kutafsiri  ushuhuda  wa  Mungu. Kwa upendo, Mungu alitoa ufunuo  maalum kumhusu ili kutusaidia kupata majibu juu ya maswali hayo. Kupitia Agano la Kale na Agano Jipya, amejifunua kwetu, amejidhihirisha pasipo kuacha swali juu ya tabia yake ya upendo. Awali, ufunuo ulikuja kupitia manabii, bali ufunuo wake kamili ulitufikia kupitia Yesu Kristo (Ebr.1:1, 2). Biblia inayo matamko kuhusu ukweli ulioko kwa Mungu na kumdhihirisha Mungu kama nafsi. Mafunuo yote ni muhimu. Twahitaji kumjua Mungu kupitia Yesu Kristo (Yoh.17:3) na ukweli ulio katika Yesu (Efe.4:21). Kupitia Maandiko, Mungu anavunja vizuizi vya kiakili, kimauti na kiroho, akiwasilisha hamu yake kubwa kutuokoa.

Lengo la Maandiko Matakatifu

Biblia humfunua Mungu na kumweka wazi mwanadamu. Huweka wazi tatizo letu na suluhisho lake. Hutuwasilisha kuwa ni waliopotea, tuliokosana na Mungu na humfunua Yesu kuwa ndiye anayetutafuta na kuturudisha kwa Mungu. Yesu Kristo ndiye lengo la Maandiko Matakatifu. Agano la Kale linaelezea kuwa Mwana wa Mungu ni Masihi, Mkombozi wa Ulimwengu;  Agano  Jipya  lamfunua Yesu Kristo kuwa  ni  mwokozi.  Kila kitabu  cha  Bibila kupitia kielelezo au vinginevyo, huonesha kipengele cha kazi yake na tabia yake. Kifo cha Yesu msalabani ndio ufunuo wa hali ya juu wa upendo wa Mungu kwa mwanadamu mdhambi.

Msalaba hufanya ufunuo kufikia vilele vyake kwa kuwa huleta pamoja pande mbili zinazopingana – uovu wa mwanadamu usiolinganishwa na chochote, na upendo wa Mungu usiokwisha.  Ni  nini  zaidi  ambacho  kingefunua  upendo  wa  Mungu  kwa  mwanadamu? Msalaba unaeleza kuwa Mungu kwa kuupenda ulimwengu aliruhusu mtoto wake afe. Ni kujinyima na kafara ya namna gani? Dhamira ya Mungu kama ilivyoonyeshwa na kifo cha Yesu  Kalvari, ukweli mkuu kwa ulimwengu ndilo lengo mahsusi la Biblia na kwa mtazamo huo, twapaswa kujifunza Biblia.

Uandishi wa Biblia

Mamlaka ya Biblia kwa imani na matendo inaibukia kwenye asili yake. Waandishi wa Biblia walitofautisha Biblia na maandishi mengine. Waliita “Maandiko Matakatifu” (Rum. 1:2) Maandiko (2Tim. 3:15), Mausia ya Mungu (Rum. 3:2), Maneno ya Mungu (Ebr. 5:12).

Utofauti wa Biblia unatokana na uasili wake na chanzo chake. Waandishi wa Biblia walidai hawakuwa chanzo cha ujumbe waliouandika, bali walipokea kutoka kwa Mungu walichoandika. Ni kupitia ufunuo ndipo walipoweza kuuona ukweli walioufundisha. (Angalia Isa. 1:1; Amo. 1:1; Mik. 1:1; Hab. 1:1; Yer. 38:21). Waandishi hawa walionesha Roho Mtakatifu kuwa ndiye aliyewasiliana na watu kupitia manabii (Neh. 9:30; cf. Zak. 7:12). Daudi alisema Roho ya Bwana ilinena ndani yangu na neno lake likawa ulimini mwangu (2 Sam 23:2). Ezekieli aliandika, “roho ikaniingia, ikaniangukia, ikaniinua(Eze:2:2; 11:5, 24) na Mika anashuhudia “nimejaa nguvu kwa roho ya Bwana (Mik. 3:8).

Agano jipya linatambua jukumu la Roho Mtakatifu katika kuandika Agano la Kale.Yesu anasema Daudi alikuwa amevuviwa (Mk. 12:36). Paulo aliamini Roho Mtakatifu aliongea kupitia Isaya (Mdo. 28:5). Petro anadhihirisha kwamba Roho Mtakatifu aliongoza manabii wote, siyo wachache (1Pet.1:10, 11; 2Pet. 1:21).  Nyakati zingine mwandishi alififia akapotea na mwandishi halisi Roho Mtakatifu alikaririwa, Roho Mtakatifu anenavyo (Ebr. 3:7; 9:8). Waandishi  wa  Agano  jipya  nao  wanakiri  kuwa  Roho  Mtakatifu  ndiye  aliye  chanzo  cha ujumbe wao. Paulo asema “Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani (1Tim. 4:1). Yohana asema alikuwa katika Roho siku ya Bwana (Uf.1:10).

Na Yesu aliwapa utume wanafunzi wake kwa Roho Mtakatifu (Mdo.1:2, cf Efe. 3:3-5). Kwa hiyo Mungu kupitia nafsi ya Roho Mtakatifu amejifunua kupitia Maandiko Matakatifu.

Uvuvio wa Maandiko
Kila andiko, Paulo anena, limetolewa kwa pumzi ya Mungu (2Tim. 3:16). Neno la kigiriki theopneustos, lililotafsiriwa kuwa kuvuviwa, lina maana ya Mungu alitoa pumzi, alipulizia. Hivyo Mungu alipulizia mawazo ya wanadamu wakaweza kuwasilisha ujumbe wa Mungu.
 
Mchakato wa Uvuvio
Ufunuo  wa Mungu ulitolewa kwa wanadamu kupitia watakatifu walioongozwa na Roho Mtakatifu (2Pet. 1:21). Mafunuo yaliwekwa katika lugha ya kibinadamu. Pamoja na mapungufu yake na kasoro zake, unabaki kuwa ushuhuda wa Mungu. Mungu alivuvia watu, siyo maneno. Kuna mahali waandishi waliambiwa cha kuandika, na wakati mwingine aliwaambia waandike walichoona kwa kutumia akili zao. Paulo alizingatia Roho za Manabii huwatii manabii (1Kor. 14:32). Uvuvio halisi hauondoi hali ya aliyefunuliwa, wala akili yake, wala utu wake. Mahusiano ya Musa na Haruni yanatoa kielelezo. Nimekufanya wewe kuwa Mungu kwa Farao na Haruni atakuwa nabii wako (Kut. 7:1 cf. 4:45, 16). Musa alimjulisha Haruni ujumbe wa Mungu na Haruni kwa kutumia lugha yake na kwa mtindo aliouona unafaa,  akausema  kwa  Farao.  Hivyo,  waandishi wa  Biblia  nao  waliwasilisha  maagizo  ya Mungu, mawazo, na mausia kwa mitindo ya lugha zao.
 
Kuna mahali Mungu aliongea moja kwa moja alipotoa amri zake (Kut. 20:1- 17; 31:18 Kumb.10:4, 5). Hata hivyo, alichonena, kiliandikwa katika upungufu wa lugha ya kibinadamu. Kwa hiyo Biblia ni ukweli wa kimungu uliowasilishwa katika lugha ya kibinadamu. Kunafanana na Yesu aliyefanyika mwili (Yoh. 1:14). Muungano wa kimbingu na kibinadamu unafanya Biblia kuwa kitabu cha pekee miongoni mwa kazi zilizoandikwa.
 
Kuvuviwa na Waandishi
Roho Mtakatifu aliandaa watu kadhaa kuwasilisha ukweli wa kimbingu. Biblia haisemi waliochaguliwa walikuwa na sifa zipi. Balaam alisema ujumbe wa Mungu huku akitenda kinyume na mapenzi ya Mungu (Hes. 22 - 24). Daudi aliyetumiwa na Roho alitenda maovu ya kutisha (cf. Zab.51). Waandishi wote wa Biblia walikuwa wanadamu wenye asili ya dhambi wakihitaji neema ya Mungu kila siku (Rum. 3:12). Kuna wakati waandishi waliandika pasipo kuelewa maana halisi ya wanachoandika (1Pet.1:10-12).
Mwitikio wa waandishi kwa ujumbe walioubeba ulikuwa tofauti. Danieli na Yohana wanasema walishangazwa (Dan. 8:27; Ufu. 5:4). Waandishi wengine walichunguza maana ya ujumbe wao. (1Pet. 1:10). Wengine waliogopa kutoa ujumbe wa Mungu na wengine walibishana na Mungu (Hab. 1; Yon. 1:1-3; 4:1-11).
Namna na kinachofanyiza ufunuo
Mara kwa mara Roho Mtakatifu ufahamu wa Mungu kupitia njozi na ndoto (Hes. 12:6) Mara nyingine alizungumza akasikika katika ufahamu wa ndani (1Sam. 9:15). Zekaria alipokea vielelezo vya ishara na maelezo yake (Zek.4). Maono ya mbinguni ambayo Paulo na Yohana walipokea yaliambatana na maagizo ya kusikika (2Kor. 12:12:1- 4; Ufu. 4), Ezekieli aliona vinavyotokea upande mwingine (Eze.8). Waandishi wengine walishiriki katika matukio ya maono kama sehemu ya maono. (Ufu. 10).
 
Ufunuo mwingine ulihusu mambo ambayo hayajatokea (Dan. 2, 7, 8 na 12) Wengine waliandika  matukio  ya  kihistoria  kama  walioshuhudia  wenyewe  yaliyotokea  au  kwa kuchagua  kutoka  maandishi  kutoka  kumbukumbu  za  historia  (Waamuzi,  1  Samweli,  2 Nyakati, Injili na Matendo ya Mitume).
Uvuvio na Historia
Tamko la Biblia kwamba kila andiko lenye pumzi ya Mungu lafaa kwa mafundisho, kwa maisha ya maadili na kiroho (2Tim. 3:15, 16) haliachi swali juu ya uchaguzi wa kufundisha. Kwamba habari ilitufikia kwa kuangalia yaliyotukia, masimulizi au kazi zilizoandikwa au ufunuo wa moja kwa moja vyote yalimfikia mwandishi kwa uvuvio wa Roho Mtakatifu.
Mungu anafunua mpango wake katika kushughulika na mwanadamu. Kuaminika kwa maelezo yake ya kihistoria ni muhimu kwa sababu hutoa msingi wa kuelewa tabia ya Mungu na makusudi aliyonayo kwetu. Tukielewa kwa usahihi hutuongoza kwenye uzima, na tusipoelewa, tutapotea na kufa. Mungu aliagiza watu kadhaa kuandika alivyoshughulika na Israeli, tofauti na wengine wanavyoandika historia. Maelezo yao yanafanya sehemu ya Biblia (cf.  Hes.  33:1,  2;  Yosh.  24:25,  26;  Eze.  24:2).  Hutupatia  historia  yenye  msimamo  wa kimbingu. Matukio ya kihistoria ni vielelezo vilivyotolewa kwa kutuonya tuliofikiliwa na miisho ya zamani (1Kor. 10:11). Paulo anasema viliandikwa kwa subira na kututia moyo tupate tumaini (Rum. 15:4). Kuangamia Sodoma na Gomora ni mfano unaoonya (2Pet. 2:6, Yud. 7). Uzoefu wa Ibrahimu wa kuhesabiwa haki ni mfano kwa kila muumini (Rum. 4:1-25); Yak. 2:14-22). Hata sheria za kiserikali za zamani zina mafao kwetu (1Kor.9:8, 9).
Luka aliandika ili tupate uhakika kwa yale tuliyofundishwa (Luk. 1:4). Yohana anasema yaliyochaguliwa yanalenga kusaidia tuamini Yesu ni Kristo tupate uzima katika jina lake (Yoh.20:31). Wenye mashaka wa leo hawaamini habari za Adamu na Hawa, gharika na Yona lakini Yesu alikubali kuwa ni historia sahihi na yenye mafundisho kiroho. (Mt.12:39-41; 19:4-6; 24:37:37-39). Biblia haifundishi uvuvio wa vipengele au viwango vya uvuvio. Yote, ilivuviwa na Roho Mtakatifu.
 
Usahihi wa Maandiko
Kama  tu  Yesu  alivyofanyika  mwili  akakaa  kwetu  (Yoh.  1:14),  ili  tuelewe  ukweli,  Biblia ilitolewa katika lugha ya kibinadamu. Uvuvio wa Maandiko unatoa dhamana ya uhakika wake. Mwonekano wa kimakosa usimomonyoe kuiamini Biblia. Mara nyingi ni matokeo ya uelewa wetu finyu kuliko makosa. Pamoja na juhudi iliyofanywa kuiharibu, bado Biblia imehifadhiwa kwa usahihi wa kushangaza. Magombo yaliyotoka Bahari ya Wafu (Dead Sea scrolls) umedhihirisha uangalifu uliotumika kuinakili.
 
Mamlaka ya Maandiko Matakatifu
Maandiko  yana  mamlaka  ya  Mungu  kwa  kuwa  Mungu  amezungumza  kupitia  Roho Mtakatifu. Hivyo Biblia ni neno la Mungu lililoandikwa. Madai hayo yana ushahidi na kutupatia mwelekeo wa maisha.
 
Madai kutoka Maandiko yenyewe
Waandishi wa Biblia hudai kuwa ujumbe wao ulitoka moja kwa moja kwa Mungu. Ni neno la
BWANA, lililomjia Yeremia, Ezekieli, Hosea na wengine (Yer.1:1, 2, 9; Eze. 1:3; Hos. 1:1; Yoe.1:1; Yon. 1:1). Wakiwa wajumbe wa Bwana (Hag. 1:13; 2Nyak. 36:16) manabii waliamriwa kusema kwa jina la BWANA wakisema: Hivi ndivyo asemavyo Bwana (Eze. 2:4; cf Isa. 7:7). Maneno yake yana utambulisho wa kimbingu na mamlaka yake.  Bwana ndiye mtendaji na nabii ni mjumbe tu (Mt. 1:22). Petro anayapa hadhi maandiko ya Paulo sawa na Maandiko Matakatifu (2Pet. 3:15, 16). Paulo asema hakupokea kutoka kwa wanadamu bali kwa ni ufunuo wa Yesu Kristo (Gal. 1:12). Waandishi wa Agano Jipya waliyakubali maneno ya Yesu kuwa maandiko yakiwa na mamlaka sawa na Agano la Kale (1Tim. 5:18; Luk. 10:7)
Yesu na Mamlaka ya Maandiko
Katika huduma yake yote, Yesu alisisitiza Mamlaka ya Maandiko. Alipojaribiwa na Shetani au alipopambana na wapinzani wake “imeandikwa” ndiyo ilikuwa utetezi wake (Mt. 4:4, 7, 10; Luk. 20:17). Mwanadamu hataishi kwa mkate tu, bali kwa neno la Mungu (Mt. 4:4). Alipoulizwa jinsi gani mtu ataingia ufalme wa Mungu yeye alijibu imeandikwaje katika torati (Luk. 10:26). Yesu aliiweka Biblia juu ya mapokeo ya wanadamu na kuwakemea walioweka pembeni mamlaka ya Biblia (Mk. 7:7-9). Aliwaalika wanadamu kuisoma Biblia kwa uangalifu (Mt. 21:42, cf. Mk. 12:10, 26). Aliamini kwa nguvu zote kuwa maandiko yalimshuhudia (Yoh.5:39, 46). Yesu aliamini utume wake ulizungumziwa katika Agano la Kale (Luk.24:25-27). Hivyo pasipo kubabaika wala kubakiza kitu, Yesu alikubali Maandiko Matakatifu kuwa ufunuo wenye mamlaka wa mapenzi ya Mungu kwa mwanadamu.
 
Roho Mtakatifu na Mamlaka ya Biblia
Wakati wa maisha ya Yesu duniani viongozi wa kidini hawakumtambua. Wengine walidhania alikuwa nabii kama Yohana Mbatizaji, Eliya au Yeremia – yaani mwanadamu tu. Petro alipokiri kuwa ni Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai, Yesu alisema huo haukuwa ufunuo wa kibinadamu bali wa kimungu (Mt. 16:13-17). Paulo alisisitiza hakuna awezaye kusema Yesu ni Bwana isipokuwa katika Roho Mtakatifu (1Kor. 12:3) Hakuna ajuaye ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu (1Kor.2:11). Akili ya kawaida ya kibinadamu haiwezi kupokea mambo ya kiroho kwa kuwa hutambulika kiroho (1Kor. 2:14). Kwa namna hiyo, msalaba ni upuuzi kwa wanaopotea (1Kor. 1:18). Ni kupitia Roho Mtakatifu peke yake awezaye kuchunguza mambo ya Mungu (1Kor. 1:10) ndipo mtu aweza kuamini juu ya Mamlaka ya Biblia. Sasa tumepokea siyo roho wa dunia bali Roho atokaye kwa Mungu tuyatambue yaliyotolewa kwetu (1Kor.2:12). Mamlaka ya Biblia kwenye maisha yetu huongezeka au kupungua kwa kulingana na vile tunavyoelewa kuvuviwa na Roho Mtakatifu. Mafundisho yake yatakubalika kufaa kwa mafundisho na kuonya ikiwa tutaamini uvuvio wake (2Tim. 3:16).
Kiwango cha Mamlaka ya Mandiko Matakatifu
Hekima yote ya kibinadamu lazima iitii mamlaka ya Biblia. Biblia haipaswi kuwekwa chini ya kawaida za kibinadamu. Ni bora kuliko hekima na maandishi yote ya kibinadamu. Maandiko yanadumisha mamlaka juu ya karama za Roho juu ya unabii au kunena kwa lugha (1Kor. 12; 14:1; Efe. 4:7-16). Karama za Roho haziondoi mamlaka ya Biblia badala yake yote yapaswa kupimwa kwa Maandiko – na waende kwa sheria na ushuhuda (Isa. 8:20).
Umoja wa Maandiko Matakatifu
Kusoma kijuujuu kutaleta uelewa wa kijujuu.  Mungu hakujifunua kwetu kwa mfululizo wa maagizo bali amejifunua kidogo kidogo kupitia mfuatano wa vizazi, kwamba ni kwa Musa kwenye nyika ya Midiani au kwa Paulo akiwa gerezani. Pamoja na kuandikwa kwa vizazi vingi,  bado  Agano  la  Kale  na  Agano  Jipya  haviwezi  kutenganishwa.  Mungu  ametualika tumjue kwa kusoma Maandiko na kukamilishwa na kupewa uwezo wa kutenda mema (2Tim.3:16