Viongozi NETC Waokoka na Ajali

Posted on Apr 27 2019

Na Almodad Amos
Habari NETC | Same

Watendakazi na washiriki wa Kanisa la Waadventista Wasabato NETC tuungane katika kumshukuru Mungu kwa kile ambacho Mchungaji Nzumbi (Katibu Mkuu wa Konferensi) amekiita Kuokolewa na Malaika aliyetumwa na Mungu katika ajali mbaya iliyotokea wakati Menyekiti - Mchungaji Elias Ijiko, Muhazini - Eld. Emmanuel Tuarira, Katibu Mchungaji Musa Nzumbi na Mch. John Kimbute; wakiwa safarini kurejea Same baada ya majukumu mbalimbali ya kiofisi waliyokuwanayo.

Akizungumza katika kutoa ushuhuda wa jinsi walivyookoka, Mwenyekiti wa Konferensi Mchungaji Elias Ijiko amesema "Nimesikia mtu akisema wimbo wa amatenda maajabu nami siwezi kueleza, unapaswa kuimbwa kwa kusema nami naweza kueleza; lakini mimi nasema, ikiwa unaweza kueleza hiyo si ajabu. Mungu ametutendea maajabu wala hatuwezi kueleza."

Hapa ni Mchungaji Musa Nzumbi akisimulia jinsi ajali hiyo mbaya ilivyotokea kwa kile walichoshuhudia:Hapa chini ni picha za gari baada ya ajali: