Kugawanya Konferensi Leo

Posted on Jan 03 2019


Na Almodad Amos
Habari NETC | Same

Kumekuwa na vuguvugu la makusudi mema ya kuigawanya Konferensi ya North East Tanzania Conference kwa muda muda mrefu na sasa inaonekana kuwa leo hii tarehe 03 Januari 2019 makusudi hayo yanaweza yakafikiwa katika vikao maalum vya Union ya NTUC.

Konferensi ya NETC inaonekana kuwa kubwa sana ikiwa na mikoa minne inayochukua Tanga, Kilimanjaro, Arusha na Manyara. Hata hivyo inahudumia makanisa baadhi ya makanisa ambayo yako mkoani Singida. Ukubwa huu wa Konferensi umeonekana kuwa na changamoto katika harakati za viongozi wa Konferensi ya NETC kukidhi mahitaji ya makanisa kufikiwa kihuduma, na ofisi zake.

Hitaji hili linaonekana kuwa limekuwa mojawapo ya sababu zilizopelekea kamati Kuu ya Union kukutana leo kule jijini Arusha na kuona namna ya kufanya maamuzi yatayofanya mustakabali wa mpango huu. Akitoa taarifa yake Mwenyekiti wa Konferensi katika kikao cha mwisho wa mwaka 2018, alitoa maendeleo ya mchakato huu na mapendekezo maalum ya kile kinachotarajiwa katika mgawanyo, kama sehemu ya taarifa hiyo inavyoonekana katika video hii:Endelea kufuftilia Habari NETC, tutakujuza zaidi mara tu habari hizi zitakapokuwa bayana na kuwekwa wazi zaidi kuhusu maamuzi ya mwisho yatakayofanywa